Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Baadhi ya wafuasi wa chama cha upinzani cha CORD wameunga mkono hatua ya baraza kuu la muungano huo ya kutaka kuwafurusha wabunge waasi wa chama hicho ambao wanaendelea kuonyesha nia ya kuunga mkono chama cha utawala cha Jubilee.

Wenyeji hao ambao waliongea kwenye soko kuu la Marikiti jijini Mombasa walisema kuwa wabunge hao wanahitajika kufutiliwa mbali na kusimama upya kuwania kiti cha ubunge wakitumia chama ambacho wanapendelea kwa sasa.

Akiongea na na makala haya siku ya Alhamisi, Said Abubakar ambaye ana nia ya kuwania kiti cha uwakilishi wadi katika kaunti hiyo, alisema kuwa wakati umefika kiongozi yeyote ambaye anaonyesha ukosefu wa imani na chama kilichompa nafasi ya kuingia bungeni kutemwa kutoka chamani.

Alisema kuwa hatua ya kuandikiwa barua kwa viongozi wawili Gideoni Mung’aro na Mwenzake Mustafa Iddi ni kuonyesha kuwa maslahi ya ufuasi wa chama ni muhimu kuliko ya watu binafsi ambao wanataka kutumia nafasi yao ya uongozi kwa manufaa yao ya ubinafsi.