Kuna wagonjwa wapatao 187 hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi MTRH mjini Eldoret wanaosubiri kuwekwa figo.
Afisa mkuu wa hospitali hiyo dakta John Kibosia alisema tayari hospitali hiyo imetoa mafunzo kwa madaktari na wataalam wengine ambao watakuwa wakiendeleza shughuli za kuwekea wagonjwa husika figo.
“Kutokana na mafunzo ambayo madaktari hawa awapepokea kuhusu mchakato mzima wa kuwekea wagonjwa figo itakuwa rahisi kuendeleza shughuli hii kila siku katika hospitali hii ambayo ianahudumia wagonjwa kutoka kanda nzima ya Magharibi mwa Kenya na matiafa jirani kama vile Uganda,Tanzania na Sudan Kusini,” alisema Dkt Kibosia.
Daktari Kibosia alisema ufanisi huo umeafikiwa kupitia ushirikiano kati ya hospitali hiyo na madaktari kutoka Uholanzi ambao ni wataalam wa tajiliba ya juu katika maswala ya uwekaji figo.
Ushirikiano huo ulihusisha masomo kuhusu mbinu za kuwekea figo wagonjwa amabao figo zao huwa zimefeli,kutunza wagonjwa hao miongoni mwa huudma nyingine za kiafya ambazo ni muhimu kwa wagonjwa hao.
Bw Kibosia alifichua kuwa hospitali hiyo ina mipango ya kutuma madaktari zaidi Afrika kusini kupokea mafunzo zaidi kuhusu maswala ya kuhudumia wagonjwa ambao wanachangamoto ya kufeli kwa figo.
Daktari Kibosia alisema kutokana na kuimarika kwa huduma hizo hospitalini humo kuna ongezeko la wagonjwa ambao hufika hospitalini humo wakitafuta huduma hiyo.
Akihutubia wanahabari hospitalini humo kuhusu mikakati ya kuimarisha huduma hiyo Dkt Kibosia alisema gharama ya kuwekea figo hospitalini humo kwa mtu mmoja ni shilingi 30,000 ambapo wagonjwa ambao wamejisajili na bima ya kitiafa ya afya NHIF watakuwa wakilipa shingi 150,000 ambapo bima hiyo itakuwa ikilipia pesa zilizosalia.
“Ningependa kushauri wagonjwa ambao wangependa kuwekewa figo kutembea hospitali hii kwa huduma bora kwa malipo nafuu badala ya kutafuta huduma hizo katika matiafa ya kigeni ambayo hulipisha kati ya shilingi milioni3 na milioni 4 kwa huduma sawa,” alisema Dkt Kibosia.