Mwenyekiti wa bodi ya kuthibiti ukeketaji wa wasichana nchini Jebii Kilimo amewaonya wahudumu wa afya katika eneo la Gusii dhidi ya kuendeleza tabia hiyo, huku akionya kuwa watafunguliwa mashtaka. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubu kwenye hafla ya kufuzu kwa wasichana 120 kule Nyamira siku ya Jumanne wakati wasichana waliokuwa wakipokea mafunzo ya jinsi ya kuvuka daraja la utu uzima bila ya kukeketwa kupitia kwa udhamini wa shirika la Vinbell Foundation, Kilimo alisema kuwa afisa yeyote wa afya atakayepatikana na hatia ya kuwakeketa wasichana atafungwa kifungo cha miaka mitatu. 

"Afisa yeyote wa afya atakayepatikana na hatia ya kuwakeketa wasichana atafungwa kifungo cha miaka mitatu na huenda akaachishwa kazi kwa kuwa ni hatia kisheria kuwaketa wasichana nchini," alionya Kilimo. 

Kilimo aidha aliwapongeza wazazi walioruhusu watoto wao wasichana kuhudhuria kongamano hilo la mafunzo hayo ya siku kumi, huku akiongeza kuwa viwango vya ukeketaji katika maeneo mengi Gusii vinastahili kuangaziwa ili vithibitiwe. 

"Ningependa kuwashukuru wazazi waliochukua hatua ya kuwaleta wanao kwenye hafla hii ya kupata mafunzo ya jinsi ya kuvuka daraja la utu uzima, ila kutokana na asilimia 98% ya visa vya ukeketaji wa wasichana kuendelea kukithiri katika maeneo mengi Gusii, ningependa mashirika yote ya kijamii yashirikiane ili kuhakikisha kuwa visa hivi vimepunguzwa," alihoji Kilimo.