Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baada ya msongamano mkubwa wa magari kushuhudiwa katika mji wa Kisii, maafisa wa trafiki wameombwa kuinglia kati na kupunguza hali hiyo, ambayo hufanyika sana wakati wa asubuhi na wakati jioni.

Hali hiyo ilifikia viwango vya kutatanisha hii leo, Ijumaa, ikiwa ndio siku ya wanafunzi wa chuo cha Kisii walikua wanahitimu rasmi, ambapo msongamano mkubwa ulishuhudiwa. 

Wakizungumza na waandishi wa habari, wahudumu wa matatu mjini humo, wakiongozwa na Aloyce Moti, waliwataka maafisa wa trafiki mjini humo kuboresha uelekezaji wa magari kwenye barabara za mji huo haswa zile hukumbwa na msongamano mwingi nyakati za asubuhi na jioni na hata mchana kwa kila siku.

Kulingana na wahudumu hao, uelekezaji wa trafiki unahitajika mjini humo ili kupunguza misongamano hiyo kwani kuna baadhi ya waendesha magari hawazingatii sheria za barabarani na kupitisha magari mahala hakustahili.

“Barabara zinazoingia steji ya Kisii huwa na misongamano mikubwa ambayo husababisha foleni ndefu ya magari kila siku kufuatia ukosefu wa uelekezi wa maafisa wa trafiki, na tunaomba maafisa hao waje ili kutusaidia,” alisema Moti.

Wakati uo huo, wahudumu hao waliomba serikali kupanua barabara za mji huo ili kupunguza misongamanao hiyo ya magari inayoendelea kushuhudiwakila mara.