Wahudumu wa pikipiki mjini Eldoret waliandamana mnamo siku ya Jumatatu asubui kufuatia kugongwa na kuuliwa kwa mmoja wako usiku wa kuamkia Jumatatu katika eneo la Poles kwenye barabara kuu ya Uganda Road.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Jeremiah Nyaosa, wahudumu hao waligadhabika sana baada ya dereva aliyetekeleza kitendo hicho kuachiliwa na maafisa wa polisi bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria.

Wahudumu hao walipiga kambi nje ya ofisi ya kamishena wa Kaunti ya Uasin Gishu, Hassan Abdi wakitarajia kumuona uyo kamishena ili apokee malalamiko yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Nyaosa alilalamika kuwa wahudumu wa pikipiki wamekua wakinyanyaswa na kutohakikishiwa usalama na maafisa wa polisi, jambo ambalo limesababisha uadui kati ya vikundo hivyo viwili.

"Maafisa wa polisi wamekua kama maadui kwa wahudumu wa pikipiki na tunashuku ya kwamba ndio sababu wamemwachilia dereva aliyemgonga na kumuangamiza mmoja wetu bila kumchukulia hatua yoyote ya kisheria," aliteta Nyaosa.

Haya yalitendeka juma moja ju baada ya wahudumu hao hao, wakishirikiana na waendeshaji taxi, kuteta kwamba komishena wa polisi na maafisa wengine mjini Eldoret wamekua wakiwanyanyasa na kuwaitisha hongo zinazozidi mapato yao ya kila siku.

Wahudumu hao walisema ya kwamba wangependa kuwa na mkutano na kamishena wa Uasin Gishu pamoja na maafika wa polisi ili kutafuta suluhu la kudumu na kuangamiza uadui baina yao na maafisa wa polisi.