Waislamu katika Kaunti ya Mombasa wameelezea kuridhishwa na ujumbe wa Papa Francis, na kumpongeza mwenyekiti wa baraza la waislamu nchini Supkem Abdulghafur El-Busaidy kwa kutoa ujumbe wenye maadhi ya mshikamano wa dini mbali mbali nchini.
Wakiongozwa siku ya Alhamisi na Sheikh Samir Hassan katika eneo la Kizingo jijini Mombasa, wenyeji hao wa Mombasa walisema wakati umefika viongozi wa kisiasa kuiga mfano wa viongozi wa makanisa na misikiti vile ilifanyika siku ya Alhamisi ambapo makasisi, masheikh pamoja na wahubiri wa madhehebu mbalimbali katika ziara ya Papa Francis.
Samir pia alichukua wakati wake kumusifia kiongozi wa SUPKEM Profesa Abdulghafur El-Busaidy Jinsi alivyowasilisha ujumbe kwa niaba ya Jumuia na dini nzima ya waumini wa kiislamu, na kusema kuwa ujumbe huo uliwakilisha barabara matakwa ya kila muumini wa dini hiyo.
Aidha aliongeza kuwa wapo tayari siku zote kushikana mkono na waumini wa dini nyingine ili kuunganisha wakenya na kujaribu kutokomeza dhana za utengamano na nguvu ambazo zinalenga kubomoa mshikamano ulioko baina ya madhehebu yote nchni.
“Kila mkenya anahitaji kuuchukulia mkutano wa leo kwa uzito unaostahili, na kiongozi wa nchi kufuata hekima ya kiongozi wa dini ya kikatoliki nchini Baba Francis, vile aliwarai wote kuendelea kuimarisha uhjusiano wa kudumu na dini zote kustahimiliana,” alisema Samir,