Wajane wa aliyekuwa mwanasisasa wa Nakuru Dickson Kihika Kimani wamempa spika wa bunge la kaunti ya Nakuru Susan Kihika makataa ya siku saba kuwaomba msamaha kwa madai kwamba anawakosea heshima.
Wajane hao wamemshtumu Spika Kihika kwa kuwahangaisha na wanamtaka achapishe taarifa ya kuomba msamaha kwenye magazeti ya kitaifa humu nchini.
Kwa mujibu wa mwanaye mjane mkongwe wa Kihika, Hellen Wangare, spika wa kaunti ya Nakuru amesababisha mzozo kuibuka kuhusiana na urithi wa mali ya marehemu Kihika Kimani.
Wangare anasema kuwa hawajafurahia kwamba swala hilo la familia ya Kihika limekuwa katika vyombo vya habari na hata umma.
Familia sasa inamrai Spika Kihika Kimani kushirikiana nao katika kutatua swala hilo mara moja.
Hata hivyo,katika taarifa kwa vyombo vya habari, spika Susan Kihika alisema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri ambao wanaingilia swala hilo kando na kuwa ni la kifamilia.