Wakaazi wa Elburgon wamefanya maandamano wakiteta kuhusu kutekwa nyara kwa mfanyibiashara mmoja wa eneo hilo.
Inaarifiwa kuwa mkaazi huyo ambaye alikuwa ni mhudumu wa bodaboda alitoweka siku ya Jumapili na hajulikani aliko.
“Polisi wamekosa kusaidia katika uchunguzi wa mmoja wetu. Kwa nini hakuna hatua zozote ambazo zimepigwa?” alisema John Kamau. Kamau alisema jamaa huyo ambaye anajulikana kama Maina Githinji alitoweka siku tatu zilizopita na hakuna hatua imepigwa.
“Tunataka polisi waeleze ni kwa nini hakuna hatua wanachukua licha ya wananchi kupiga ripoti,” mkaazi mwingine alisema.
Maandamano hayo yalitatiza usafiri kwenye barabara ya Elburgon-Molo.