Share news tips with us here at Hivisasa

Kulishuhudiwa giza totoro mjini Mombasa siku ya Alhamisi usiku baada ya umeme kupotea kwa muda mrefu.

Kulingana na kampuni ya umeme nchini Kenya Power, miji ya Mombasa, Nairobi na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kati, yalitarajiwa kukosa umeme siku ya Alhamisi kuanzia saa 4:30 jioni.

Katika taarifa yake, Kenya Power, ilisema kuwa kulikua na tatizo katika mashine zake zilizoko stesheni ndogo ya Juja, mjini Nairobi.

Giza hiyo ilitatiza shughuli za biashara ambapo wakaazi na wafanyibiashara walilazimika kufunga biashara zao mapema kwa kuhofia kuibiwa.