Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa Mombasa wanapongeza hatua ya Rais Kenyatta kudinda kuteua jopo maalum la kumchunguza jaji wa mahakama ya juu Philip Tunoi.

Hii ni kwenye kesi ya kupokea hongo ya shilingi milioni 200 kutoka kwa gavana wa Nairobi Evans Kidero.

Wakazi hao wameseme kuwa raisi ameonyesha kuwa na msimamo dhabiti na idara ya mahakama nchini kwa kukata kuunda jopo hilo la kunchunguza Tunoi.

Abdalla Suleiman, mkazi wa Mshomoroni,alisema siku ya Jumatatu ,kuwa serikili inafaa kuja na mbinu mwafaka ya kukomesha visa vya ufisadi wala si kuunda majopo maalumu ambayo mwishowe yanapaswa kulipwa kutoka kwa fedha za umma.

Ikulu ya rais ilisema kuwa rais Uhuru Kenyatta, hatoteuwa jopo maalumu la kumchunguza jaji wa mahakama ya juu ,Philip Tunoi kuhusiana na sakata ya ufisadi ya shilingi milioni 200 hadi pale mahakama ya rufaa itakapotoa uamuzi kuhusu kesi ya umri wa kustafu kwa jaji huyo wa mahakama ya juu.

Mkuu wa watumishi wa umma Joseph Kinyua amesema haitakuwa na maana kuundwa kwa jopo hilo litakalotathmini kuondolewa kwa Tunoi iwapo mahakama ya rufaa itaamuwa aondoke mamlakani akiwa na miaka 70 kulingana na kesi ya umri wake.

Mnamo Februari 9,2016,tume ya idara ya mahakama ilipendekeza rais Kenyata kuunda jopo maalumu la kumchunguza kuhusu sakata ya shilingi milioni 200 anazodaiwa kupokea kutoka kwa gavana wa Nairobi Eevans Kidero ili kupata kupendelewa katika kesi ya uchaguzi wa mwaka 2013 iliyowasilishwa na mpinzani wake Ferdinand Waititu.