Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi wa Naivasha wameteta kuhusu ongezeko la wizi wa mifugo kwenye eneo hilo.

Wakaazi walisema wengi wa wakaazi wamepoteza ng’ombe na kondoo kupitia wizi huo.

“Wakaazi hapa wamepoteza mali nyingi sana. Ng’ombe na Kondoo zinaibiwa hapa kila siku na hazipatikani hata baada ya kuwahusisha maafisa wa polisi,” George Mwaniki alisema.

MCA wa Lake View Simon Wanango amewalaumu maafisa wa polisi katika kitengo cha antistock theft kwa kile alisema ni utepetevu kazini.

“Hawa wakazi wanataabika sana. Wengi hapa mali yao imeibiwa na hawa stock hawajasaidia,” Wanango alisema siku ya Jumatano.