Askofu Maurice Makumba wa jimbo katoliki la Nakuru ametoa wito kwa wakristo na wakaazi wa Nakuru kwa jumla kudumisha amani hasa msimu huu wa krismasi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katika ujumbe wake wa krismasi, kiongozi huyo wa kidini alisema kuwa kando na shamra shamra za krismasi, kuna umuhimu wa wakaazi kudumisha amani.

Askofu Makumba vile vile alitoa wito kwa wakaazi kuwajali wasiyojiweza katika jamii.

Akizungumza katika Gereza kuu la Nakuru wakati alipowatembelea wafungwa siku ya Jumanne, Askofu Makumba aliitaka jamii kuwakumbatia wafungwa wanaporejea katika jamii baada ya kukamilisha kifungo chao.

Wafungwa hao walikabidhiwa bidhaa mbalimbali kama zawadi za krismasi.