Wakaazi mtaani Kivumbini Nakuru wanajivunia kwa kupakana na mbuga ya kitaifa ya Nakuru ambapo kila majira ya jioni wao hufurahia kutazama mandhari ya mbuga hiyo ikiwemo wanyama.
Kelvin Mbuguà ambaye ni mkaazi wa mtaa huu anasema kwa kawaida mtu hulazimika kulipa ada fulani ya kiingilio,lakini kwao hali sivyo kwani wanapakana na mbuga hiyo.
"Sisi tuna bahati sana manake tunaweza hata tazama wanyama majira ya jioni wakati kama nyati wanapokuja kula karibu na hii sengenge," Mbugua alisema.
Kwa mujibu wake, kuishi kwao karibu na mbuga hii ya Nakuru ni kwa manufaa sana hata kwa watoto wao.
Hata hivyo, katika mahojiano na mzee wa kijiji Kinuthia wa Mwangi amewataka wazazi kutowaruhusu watoto wao kuwakaribia wanysma hao.
Kinuthia alisema kuwa kando na mbuga kuwakaribia wazazi wanafaa kujihadhari.
"Tunajua sisi ni majirani wa mbuga hii lakini tafadhali wazazi tusiruhusu tu watoto kukaribia ua la mbuga hii," Mbugua alisema.