Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Jubilee imepongezwa na wakaazi wa kaunti ya Nakuru kwa kutoa kandarasi za mradi wa kuwapa watoto vipatakalishi ambavyo vitaanza kutolewa kwa shule mwezi Juni 2016.

Mnamo Jumanne vyuo vikuu vya JKUAT, kile cha Moi pamoja na washirika wao, walitangazwa na serikali kama washindi wa kandarasi hizo.

Kulingana na mkaazi Ebeneza Kinyozi kutoka Kabatini, ni kwamba serikali ya Jubilee hatimaye imetimiza ahadi yake ya kuwapa wanafunzi wa darasa la kwanza vipatakalishi, na kudhihirisha uongozi wa “kusema na kutenda”.

 Paul Munyua, mzazi wa mwanafunzi mmoja katika shule ya St Antony Heshima, alipongeza serikali akisema kwamba kufeli kwa mradi huo ingekuwa pigo kubwa kwa Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika chaguzi za 2017.

“Mimi sioni kama hii ni siasa za 2017, ilikuwa ni lazima serikali ingetimiza ahadi zake, japo ilisemekana kwamba wanafunzi wangepata vifaa hivyo kabla ya siku 100 za uongozi wa jubile," Munyua alisema.