Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Baadhi ya wakaazi Mombasa wamepinga hatua ya kuharibiwa kwa chakula kwa madai kuwa ni cha magendo.

Wakazi hao wakiongozwa na Francisi Mwaro, walionyesha kusikitishwa jinsi serikali inaharibu chakula hicho ikizingatiwa kuna wananchi wanaokubwa na uhaba wa chakula nchini.

Mwaro aliongeza kuwa heri chakula hicho kingetolewa kama msada kwa maskini ama hata kwa watoto yatima badala kuharibiwa.

Mwaro aliitaja hatua hii kama msukumo wa kisiasa hasa baada ya kufungwa kwa mabohari ya familia ya gavana Joho.

Siku ya Jumatano, mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini KRA iliharibu makasha 18 ya sukari na 49 ya mchele kwa kumwaga chakula hicho baharini.

Mchele huo wa zaidi ya tani elfu moja ulikuwa uende nchini Uganda ila mwenye mali hakujitokeza baada ya KRA kusema chakula hicho hakifai kwa mataumizi ya mwanadamu.

Aidha sukari iliyonaswa ilikuwa ya magendo na hadi sasa mamlaka hiyo inasema haijaichukulia hatua kampuni ya uhifadhi wa makasha iliyokuwa inahifadhi sukari hiyo.

Katika hotuba yake kwa wanahabari Kamishana Julius Musyoki anayeshughulika na maswala ya forodha na kudhibiti mipaka, alisema pia wameanza kuharibu makasha 63 ya kemikali ya Ethanol.

Aidha, alisisitiza kuwa wataendelea kukabiliana na biashara haramu bandarini Mombasa kwa kufunga mabohari yanayoendeleza biashara haramu pamoja na kuwafungulia mashtaka wahusika.