Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakazi katika shamba la Waitiki eneo bunge la Likoni wanamtaka raisi kuwaongezea miaka ya kulipa ada ya ardhi hiyo kwa takribani miaka 40.

Wakiongozwa na Hamisi Ali Domoko, wakazi hao wanasema kuwa kutokana na hali duni ya kiuchumi inayowakabili itakuwa changamoto kubwa kwao kulipa ada ya shilingi 182,000 kwa miaka mitatu au 12 waliyopewa na serikali.

Domoko alisisitiza kuwa miaka 40 inatosha katika kulipa ada hiyo ikilinganishwa na kipato cha wakazi wa eneo hilo ambao wengi ni wafanyibiashara wa rejareja.

Domoko ameonyesha wasiwasi kuwa kuna baadhi ya wakazi watalazimika kuhama eneo hilo kutokana na kiwango hicho cha pesa walizotengewa kulipa kwa muda mchache uliotengwa na serikali.

Raisi Kenyatta aliwaagiza wakazi wa eneo hilo kulipa ada ya shilingi 182,000 kama ada ya umiliki wa vipande vya ardhi hiyo.