Mwanasiasa kutoka eneo bunge la Kitutu Masaba amewaonya wakazi dhidi ya kupuuza tahadhari zilizotolewa kuhusu mvua ya El Nino.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza katika Kanisa la Kiadventista ya Riosiago siku ya Jumamosi, Victor Swanya, aliwaomba wakazi kuzingatia tahadhari hizo ili kujiepusha na madhara ambayo huenda yakatokea.

"Nawaomba muchukue hatua mapema kwa sababu mvua hiyo huenda ikaleta madhara mengi kwetu. Msipuuze tahadhari ambazo zimetolewa," alisema Swanya.

Vilevile, Swanya aliwaomba wakulima kutumia njia mbadala ili kuendeleza kilimo msimu huu.

"Tutumia mbinu zingine ili kuendeleza kilimo tusije tukalala njaa. Kuna madhara kadha wa kadha ambayo yatajitokeza baada ya msimu wa mvua na hayatakuwa ya kuridisha," alisema Swanya.

Mchungaji Agwata wa kanisa hilo kwa upande wake aliwaomba wazazi kuwavisha watoto wao nguo nzito kuepuka maradhi yanayosababishwa na baridi.

"Wazazi wanapaswa kuwaonya wanao dhidi ya kujikinga chini ya miti wakati wa mvua na pia wawakinge watoto kutokana na baridi kali. Tunafaa pia kuhakikisha kuwa mifugo wanalala mahali pakavu ili kuepuka magonjwa," alisema Agwata.