Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Likoni waliopewa vyeti vya kumilki ardhi wametakiwa kutouza ardhi na badala yake kuzitumia vyema kimaendeleo.

Kauli hii ilitolwa siku ya Jumanne na mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri nchini Sheikh Mohamed Khalifa katika afisi za baraza hilo.

Khalifa alipongeza Rais Kenyatta kwa kusisitiza kuwa ameonyesha mfano mzuri wa kutatua matatizo ya ardhi eneo la Pwani.

Wakati huo huo amepongeza mfumo wa mfumo wa hati miliki zilipewa wakazi kwa kuongeza kuwa mfumo huu utapunguza uzaji wa ardhi kiholela na kupunguza uskota.

Aidha, amepongeza kiwango cha pesa wanazotozwa wakazi ilikumiliki kipande cha ardhi.