Wakazi wa eneo la Mjini katika Kaunti ya Machakos waendelea kukadiria hasara baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia siku ya Jumanne.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na wakazi hao, kulishuhudiwa mafuriko kwa vile mitaro iliyoziba katika eneo hilo haijazibuliwa, jambo lilosababisha maji kuingia katika nyumba zao.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne, wakazi hao walieleza hofu ya mkurupuko wa maradhi iwapo mvua hio itaendelea kushuhudiwa, kwani maji ya mvua yanachanganyika na maji taka.

Wakazi hao waliiomba serikali ya kaunti kushughulikia swala hilo haraka ili kuzuia hasara zaidi.

"Niliamka usiku na kupata maji machafu yakiwa yamejaa katika nyumba yangu na vyombo vikiwa vimesombwa. Nahofia magonjwa yanayotokana na maji machafu huenda yakashuhudiwa iwapo mvua hii itaendelea kunyesha,” alisema Aisha Hassan, mkazi.

"Maji machafu yamezomba bidhaa zangu za dukani. Hata sijafanya biashara leo kwani nimekuwa nikitafuta njia ya kuyatoa maji haya yaliyokuwa yakizidi kadri kunyeshavyo,” alisema Bernard Mulwa, mkazi.