Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Mvita Sharrif Nassir ametoa wito kwa wakazi wa Mombasa kujisajili katika zoezi la kukata kadi za kura nchini.

Nassir alisema kuwa hatua hiyo itawapa wakazi nafasi ya kuwachagua viongozi wanaowafaa ifikapo mwaka wa 2017.

Akizungumza na wakazi katika eneo la Old Town, Nassir alisema wakazi wa Mombasa sharti wahamasishwe katika zoezi la usajili wa wapiga kura ili kuwawezesha kupata viongozi bora katika maeneo ya Mombasa.

Aidha, Nassir amewataka wakazi wa Old Town kuzingatia amani wakati huu wa usajili wa wapiga kura ili kuweza kuendeleza miradi yao mbali mbali na kukuza uchumi nchini.

Vilevile, mbunge huyo amewataka vijana kutokufa moyo kwa kusitishwa kwa mradi wa kitaifa wa vijana wa NYS baada ya sakata ya ufisadi kukita katika mradi huo.

Kulingana na mbunge huyo, vijana wanapaswa kuendelea kujisajili mashinani ili kujiweka tayari katika mradi huo, wakati utakapoendelezwa katika maeneo ya Old Town.