Mbunge wa eneo bunge la Borabu kaunti ya Nyamira Ben Momanyi amewahakikishia wakazi wanaoishi mpakani Borabu na Sotik usalama wa Kutosha baada ya kuandaa kikao na waziri wa usalama wa ndani nchini Joseph Nkaiserry na kumhakikishia kuwa atatuma maafisa wapya wa polisi katika eneo hilo na kuondoa wale walioko kwa sasa ili kuimarisha usalama.
Haya yanajiri baada ya maafisa wa polisi wa kituo cha Riotonyi kilichoko mpakani wa Borabu na Sotik kudaiwa kutowajibikia kazi yao na kupelekea wizi wa mifugo kuendelea kushuhudiwa katika eneo hilo kila siku.
Momanyi amekuwa mstari wa mbele kupigania usalama katika mpaka huo, na kudai maafisa wa polisi wa eneo hilo wamezembea kazini kwa muda mrefu kuku jamii ya mkisii ikiendela kupata hasara kubwa kwa kuibiwa mifugo wao kila wakati.
Akizungumza siku ya Alhamisi kupitia redio ya Egesa, Momanyi alisema kuwa waziri Nkaiserry alimwahakikishia kuwautma maafisa wapya wa polisi katika mpaka huo ili kuimarisha usalama.
“Huenda iwe afueni kwa wakazi wetu ambao wamekuwa wakiipigwa mifugo wao na ata vita kushuhudiwa mpani Borabu Sotik kufika mwisho maana maafisa wapya wa polisi watatumia eneo hilo,” alisema Momanyi.