Afisa kutoka Shirika la Mission in Action amesema kuwa dhuluma zozote dhidi ya watoto hazifai na yeyote atakayepatikana na hatia ya kuwadhulumu watoto anafaa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumza mjini Nakuru wakati wa mahojiano na mwandishi huyu siku ya Ijumaa, Michael Sasi alisema kuwa wakati na majira ambapo watoto walipitia dhuluma mbalimbali yamepita.
Afisa huyo alisema kuwa kwa sasa kuna sheria ambazo zinawalinda watoto na yeyote anayekiuka sheria hizo anafaa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
"Sasa sheria ipo na iko wazi kwamba watoto hawapaswi kudhulumiwa kwa njia yeyote ile. Yeyote anayewadhulumu watoto sharti achukuliwe hatua kali,”alisema Sasi.
Akigusia swala la kuasili watoto, Sasi alisema kuwa wale wote wanaonuia kufanya hivyo wanafaa kufuata sheria na kanuni zilizopo.
Sasi alisema kuwa iwapo hilo litafuatwa, basi migogoro ambayo hushuhudiwa haitakuwepo.