Wakazi wa Nakuru wametakiwa kutoa habari kuhusu wahalifu ambao wanaishi miongoni mwao ili kusaidia polisi katika vita dhidi ya uhalifu.
Akizungumza siku ya Jumanne na waandishi wa habari baada ya wezi waliokua wamejihami kwa bunduki kuuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama, afisa mkuu wa polisi kaunti ya Nakuru Hassan Barua aliwasihi wananchi kutoa habari kuhusu wahalifu wanaoishi miongoni mwao ili kusaidia polisi kukabiliana na wahalifu Mjini Nakuru.
"Nataka nichukue nafasi hii kuomba wakazi wa Nakuru kuwafichua wahalifu ambao wanaishi miongoni mwao ili kurahisisha kazi ya polisi ya kuwakamata na kuwashtaki wahalifu," alisema Barua.
Mkuu huyo wa polisi aliwataadharisha wakazi wa Nakuru dhidi ya kuwaficha wahalifu na kusema kuwa watakao patikana watachukuliwa hatua za kisheria.