Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kufuatia visa vya ukeketaji wa wasichana kuendelea kukithiri katika maeneo mengi Gusii, shirika moja linalopigania haki za wanao dhulumiwa kijinsia limejitokeza kuwahamasisha wananchi kuhusu madhara ya ukeketaji.

Akihutubu kwenye kikao cha washikadau mbalimbali katika mkahawa mmoja mjini Nyamira siku ya Alhamisi, mkurugenzi wa Shirika la Manga Art, Benard Oseko, alisema kuwa shirika hilo limeanzisha kampeni za kuwahamasisha wananchi kuwa ukeketaji huwaathiri sana kina mama ambao mara nyingi huteseka bila yakujitokeza kuelezea masaibu yanayowakumba.

"Tumeanzisha kampeni za kuwahamasisha wananchi kuhusiana na madhara ya ukeketaji kwa wasichana. Kuna idadi kubwa ya kina mama ambao wanaendelea kuteseka kutokana na changamoto zinazowakabili kutokana na ukeketaji," alisema Oseko.

Oseko aidha alisema watoto wasichana hulazimika kuacha shule baada yao kupachikwa mimba bila yakusudia hali inayo waweka kwenye hatari yakuambukizwa maradhi ya zinaa.

"Asilimia kubwa ya wasichana wamelazimika kuacha shule kutokana nakushiriki mapenzi wakiwa wangali wachanga, hali inayowaweka kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi ya zinaa,” alisem Oseko.