Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Victor Swanya, mwanasiasa kutoka Kitutu Masaba, amewahimiza wakazi kuwachagua viongozi wenye maadili mema ili kukabili visa vya ufisadi vinavyoendelea kukithiri.

Akihutubia wananchi kwenye Shule ya Upili ya Sungututa wakati wa hafla yakupokeza shule hiyo madawati, Swanya alisema kuwa kwa muda sasa wakazi wa Nyamira wamekuwa wakiwachagua viongozi wasio na maadili, hali inayo warudisha nyuma kimaendeleo.

Alisema kuwa viongozi wa aina hiyo hujihuzisha na wizi wa mali ya umma bila yakujali maslahi ya wananchi.

"Tumekuwa tukiona viongozi wafisadi wakichaguliwa kuongoza afisi mbalimbali za kisiasa, na hata idara zinazostahili kuwachunguza nakuwachukulia hatua za kisheria. Viongozi wa aina hiyo wamefeli pakubwa na sasa wakati umefika kwa wananchi kuchukua hatua yakuhakikisha viongozi wafisadi hawachaguliwi tena," alisema Swanya.

Swanya anayewania kiti cha ubunge kwenye eneo bunge la Kitutu Masaba aliwahakikishia wananchi kuwa shirika lake la Swanya Foundation litaendelea kufadhili shule mbalimbali za umma zinazokumbwa na ukosefu wa madawati.