Jamii ya Pwani imetakiwa kujumuika pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali ili kumaliza dhuluma za kijinsia.
Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto na wanawake kutoka shirika la MUHURI, Topister Juma alisema hii ni kutokana na alichokitaja kuwa ongezeko la dhuluma za kimapenzi dhidi ya watoto.
Katika mahojiano ya kipekee na mwanahabari huyu siku ya Jumatano, Juma alisema huenda taifa likakosa uongozi bora katika siku zijazo kutokana na watoto kudhulumiwa na kukosa mwelekeo maishani.
Hayo yanajiri wakati ambapo dunia nzima inaadhimisha siku 16 za utetezi wa haki za kibinadamu ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni Amani majumbani mwetu hadi dunia yote na kufanya elimu salama kwa wote.