Wakazi katika shamba la Waitiki sasa wanataka kupewa jibu moja mwafaka ambalo watalishika kuhusiana na ada ambayo ilipendekezwa wao kutoa kwa serikali na rais Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa akitoa hati miliki.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Utata huu umezuka baada ya Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kusema kuwa wakazi hao wasilipe pesa yoyote kwani shamba hilo ni la kaunti ya Mombasa, na wala si ya serikali kuu.

Joho aliyasema haya siku ya Alhamisi wakati alipokuwa akizindua mradi wa maji safi na vyoo vya kisasa katika shule ya msingi ya Mrima.

Akiongea na mwandishi huyu, mmoja wa wakazi wa eneo hilo Hirji Alfan ameelezea wasiwasi wake kwani hawaelewi wafwate yupi

“Tuna miradi yetu ya ujenzi na tumechanganyikiwa hatujui tusikize yupi,” alisema Alfan.

Matamshi yake yameungwa mkono na wakazi wengine na kumtaka Gavana Joho kusema waziwazi kila mmoja aelewe iwapo bado wanahitajika kulipa ada ya Shilingi 182,000 au la.