Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali imetenga shilingi bilioni mbili kuwafidia wakazi wa Changamwe ambao ardhi zao zitatumika kwa upanuzi wa barabara.

Haya yamebainishwa na Rais Uhuru Kenyatta wakati akizindua mradi wa barabara kuunganisha eneo la Bandari na uwanja wa ndege wa Mombasa.

Barabara hiyo ya Potrizi inapani kurahisisha uchukuzi wa mizigo, hivyo kupanua biashara baina ya taifa na nchi nyengine tegemezi kwa bandari ya Mombasa.

Barabara hiyo inayofadhiliwa na Uingereza na serikali pia inatazamiwa kupunguza msongamano wa magari katika eneo la Pwani magharibi, ambapo ukumbwa na hali mbaya wakati magari ya mizigo yakiingia bandarini na wakati huo huo magari ya kawaida yakitumia barabara hiyo.

Gavana wa Mombasa ameeleza kwamba kando na barabara hiyo kuongeza uwekezaji, pia itaboresha sekta ya utalii.