Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi wa kijiji cha Maraguishi, mjini Naivasha wanalalamikia kuharibika kwa vyakula vyao, baada ya barabara muhimu inayowasaidia wakazi hao kufungwa na bwenyenye mmoja.

Kufuatia hatua hiyo, wakazi hao, akiwemo aliyekuwa naibu wa waziri Jayne Kihara wamekosa barabara ya kuelekea Mjini Naivasha na Nairobi.

Wakazi hao pia wametishia kuharibu na kubomoa ua la stima lililowekwa na bwanyenye huyo anayedaiwa kuwa na usemi mkubwa serikalini.

Mwakilishi wadi wa eneo hilo Samuel Waithuki aidha amesema kuwa barabara hiyo imekuwa ikiwatumikia maelfu ya wakazi hao, na kuongeza kuwa hakuna sababu zozote za barabara hiyo kufungwa.

"Ujenzi wa barabara hii hufadhiliwa na serikali ya kitaifa na chakula cha mashambani husafirishwa kuelekea katika masoko ya Nairobi na Naivasha, na barabara hii inawatumikia wakazi wengi sana," Waithuki alisema.

Naye aliyekuwa Diwani wa eneo hilo Gachoka Mwaniki ameelezea kusikitishwa kwake na kusema kuwa walikuwa wakirudishwa katika enzi za ukoloni, tukio ambalo watapinga kwa vyovyote vile.