Wakazi wa eneo la Owino Uhuru wameishtaki wizara ya mazingira, kampuni ya EPZ na NEMA dhidi ya kemikali aina ya 'lead' inayoathiri afya za wakazi hao.
Wakazi hao wakiongozwa na mwanaharakati wa mazingira Phyllis Omido siku ya Jumatatu katika mahakama kuu ya Mombasa pia wamemshtaki mkuu wa washeria Githu Muigai, serikali ya kaunti ya Mombasa na kampuni ya kutengeneza vyuma kwa kushindwa kuthibiti kuenea kwa sumu hiyo.
Omido ametaka kutibiwa kwa walioathirika na kulipwa fidia, ikizingatiwa zaidi ya watu 200 waliaga dunia kutokana na sumu hiyo.
Aidha, ameongeza kuwa wakazi zaidi ya elfu 3 wameathiriwa na sumu hiyo ya Lead.