Wakazi wa eneo la Pwani wamehimizwa kufika katika vituo vya usajili wa vitambulisho na kuchukua vitambulisho vyao vya kitaifa ili kuhusika kikamilifu katika zoezi la usajili wa wapiga kura nchini.
Msajili mkuu kanda ya Pwani Aggrey Masai amesema kuwa kufikia sasa zaidi ya vitambulisho 135 elfu vimechakuliwa, huku zaidi ya vitambulisho elfu 35 vikisalia katika afisi za idara hiyo.
Akiongea na wanahabari afisini mwake mjini Mombasa siku ya Alhamis, Masai alisema kuwa kuna haja ya vitambulisho hivyo kuchukuliwa na wenyewe ili kuwawezesha kuhusika kikamilifu katika usajili wa wapiga kura.
“Tunawahimizwa vijana na wanawake kujitokeza kwa wingi na kuchukua vitambulisho vyao vya kitaifa katika vituo vyetu vya serikali na kuhakikisha kuwa wanajihusisha katika usajili wa wapiga kura nchini,” alisema Masai.
Masai amesema kuwa kaunti ya Mombasa, Kilifi na Lamu idadi kuwa ya wakazi bado hawajachukua vitambulisho vya hali ambayo ameitaja kuwa huenda ikachangia pakubwa Tume Huru ya Uchaguzi na mipika nchini IEBC ikakosa kufikia malengo yake.
“Kaunti ya Mombasa, Kilifi na Lamu bado wakazi wengi hawajajitokeza kuchukua vitambulisho, na hii ni changamoto kubwa kwa tume ya IEBC kwa sababu imelenga idadi flani ya wapiga kura kusajiliwa na iwapo watu hao watakosa kuchukua vitambulisho vyao basi watu wengi watakosa kupiga kura,” aliongeza Masai.
Wakati uo huo Masai amesema kuwa idara hiyo ya usajiliwa wa watu katika eneo la Pwani inalenga kutoa zaidi ya vitambulisho elfu 50 katika kipindi za zoezi la usajiliwa wa wapiga kura.