Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kamati ya kudhibiti vileo kwenye kaunti ndogo ya Rongai imetakiwa kuhakikisha kwamba vilabu ambavyo vinaendelea kukiuka sheria za uuzaji wa vileo havijapewa leseni.

Wito huu umetolewa na wakazi wa kutoka eneo la Ngata katika kaunti ndogo ya Rongai, kaunti ya Nakuru.

Wakizungumza na mwandishi huyu Jumapili, wakazi hao, ambao walitaka majina yao kubanwa kwa misingi ya usalama wao, walisema wafanyibiashara wengi hufungua vilabu vyao kabla ya wakati unaofaa na kufunga kama wamechelewa.

“Hapa utapata hata sasa saba viabu vingi viko wazi na shghuli zinaendelea kama kwaida, na hatujaona hatua yoyote imechukuliwa,” alisema mmoja wa wakazi hao.

Kando na hayo, wamedokeza kuwa vilabu vingi viko karibu na shule, jambo ambalo linaendelea kuathiri masomo kwa wanafunzi.

“Jambo la kuhuzunisha ni kuwa hapa kuna shule na wanaoathirika sana ni wanafunzi ambao mara nyingi tunawaona wengi wao huwa wanaingia kwa hivi vilabu,” alidokeza mwingine.

Wameitaka kamati hiyo kuzuru kwenye eneo hilo ili kushuhudia shida ambazo wanapitia.

“Tunataka NACADA ama ata Mututho mwenyewe aje ashuhudie tunayoyasema,” mwingine aliongeza.