Mvutano mkali umeibuka upya katika shamba la Waitiki, baada ya serikali ya Kaunti ya Mombasa kudai kuwa inamdai mmiliki wa ardhi hiyo shilingili milioni 400.
Hii ni baada ya serikali ya kaunti hiyo kudai kuwa fedha hizo zinatokana na ada ya mashamba ambazo zinatakikana kulipwa kila mwaka, hatua ambayo kulingana na viongozi wa serikali hiyo mmiliki huyo halali wa shamba hilo hakuwa akilipa ada hiyo.
Inasemekana kuwa mmiliki wa shamba hilo Evanson Kamau kwa jina maarufu Waitiki alisusia kulipa ada ya shamba hilo kwa mjibu wa sheria za mashamba nchini kwa serikali zilipita kwa zaidi ya miaka 20.
Mwenyekiti wa tume ya kitaifa ta ardhi nchini Mohammed Swazuri amesema kuwa wakazi wa shamba hilo huenda wakasubiri kwa siku chache, swala hilo kutatuliwa kwani wakazi hao walikuwa wanasubiri kupata hati miliki za ardhi hiyo kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta, hatua ambayo imepelekea kuhairishwa hadi siku ya Jumamosi.
Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Ijumma baada ya kutembelea shule ya msingi ya Nyali kufuatia madai kuwa sehemu ya ardhi ya shule hiyo imenyakuliwa na bwenyenye mmoja, Swazuri alisema kuwa swala hilo litatatuliwa.
"Tunawaomba wakazi katika shamba la Waitiki eneo la Likoni kuwa na subra, swala hilo tunalishughulikia na maswala ya utoaji wa hati miliki litatekelzwa," alieza Swazuri.