Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Vikwatani pamoja na maafisa wa kutetea haki za binadamu kutoka shirika la Muhuri wameandamana kupinga visa vya ubakaji katika eneo la Vikwatani.

Maandamano haya yanajiri baada ya mtoto wa miaka 12 kubakwa na kupata uja uzito katika eneo hilo.

Akizungumza kwenye maandamano hayo siku ya Alhamisi, afisa wa shirika la Muhuri Topister Juma alisema visa vya ubakaji vimezidi katika Kaunti ya Mombasa,  huku wanaohusika hawachukuliwi hatua za kisheria.

Inadaiwa msichana huyo ametoweka, na inasemekana jamaa aliyemtendea kitendo hicho ndiye aliyemtorosha.

Wakati huo huo, mkaazi wa eneo hilo Shamim Wanjala ameiomba serikali imchukulie mwanamume huyo sheria ili kupunguza visa hivyo katika eneo hilo.

Aidha, Shamim aliongezea kuwa waliripoti kesi hiyo kwa mzee wa mtaa lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa, na ndio maana wakaamua kuanzisha maandamano hayo.