Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakazi katika baadhi ya mitaa mjini Molo wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kampuni ya kusambaza maji katika kaunti ya Nakuru kuwapa maji ya mifereji na kuwaepushia taabu ya kununua bidhaa hiyo mhimu kila siku, au kutumia maji chafu kutoka kwa mito mjini humo.

Wakazi hao wamesema mifereji yao ilitoa maji mara ya mwisho mwaka wa 2006, huku wakiongeza kuwa kwa muda wa miaka 10 wamekuwa wakihangaika wanapotafuta bidhaa hiyo muhimu kwa matumizi yao ya kimsingi.

Wakazi wa mtaa wa maishani wamepongeza serikali yaKaunti ya Nakuru kwa kufanya mageuzi katika huduma za kusambaza maji, jambo ambalo limewapa afueni.

“Mara ya mwisho tulipata maji 2006, na tulilipa na tukakatiwa huduma hiyo, ni kama muujiza sasa kwamba maji yamo kwenye mifereji miaka kumi baadaye,” alisema John Mwaura, mkazi wa kitongoji cha Maishani.

“Mwaka wa 2016, Januari, na tuna maji. Hili sio jambo la kawaida, kwa vile tumekuwa tukitumia maji ya mto Molo ambayo ni chafu na yanatusababishia maradhi,” akasema Jane Kamau.

MKurungezi wa kampuni ya Nakuru Rural Water And Sanitation Company limited kutoka wilaya pana ya Molo Karanja Sonis amesema kampuni hiyo inaendeleza hatua za kuboresha usambazaji wa maji pamoja na kuweka mitambo ya kisasa ili kuhakikisha wakazi wanapata maji safi bila mgao.