Wakazi wa eneo la Majengo wameitaka serikali ya Kaunti ya Mombasa kuwafuatilia wanakandarasi waliopewa kazi ya kuzibua mabomba ya kupitisha maji na mitaro kama wanafanya kazi yao kwa njia ya sawa.
Wakazi hao ambao, waliongea na mwandishi habari huyu katika mtaa huo wa Majengo siku ya Jumatano, walisema kuwa bado miundomsingi katika mitaa si tu eneo hilo ila Kaunti nzima inavuja na maji yametapakaa kila mahali kufuatia mvua ambayo imekuwa ikinyesha tangu wiki jana ambayo imeziba mitaro.
Wakiongozwa na Leila Mwinyi, wakazi hao walalamikia serikali ya Kaunti kwa kukosa kutathmini miradi yao na kuhakikisha kuwa wanakandarasi waliopewa kazi za Kaunti wanawajibika, na kudai kuwa wengi walijukumika kutenga miundomsingi kabla ya mvua ya El Nino na wakati huu mvua hiyo inaendelea bado wanafanya kazi mbaya.
Mwinyi alisema kuwa maeneo mengi ya makazi yameingia maji, na watu wengi wamekesha kukamua maji hayo yaliyoingia majumbani, huku wakishangaa jinsi gani hela iliyotengwa kushughulikia mvua ya El Nino ilivyotumiwa.
“Serikali ya Kaunti kupitia kwa gavana wetu sharti itutengezee mitaro na kuzibua njia za kupitisha maji ya siweji na kufuatilia wanakandarasi kama wanafanya kazi yao vizuri, wengi wa wakazi wanahangaika usiku mzima kwa sababu ya maji kujaa