Wakaazi wa Nakuru wametakiwa kutumia michezo kama vile soka kuunganisha makabila yote na kudumisha amani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ni wito wake Padre Lawrence Mbogo wa kanisa katoliki Dayasisi ya Nakuru.

Akizungumza Jumatatu baada ya kushuhudia mchezo wa soka baina ya mapadre na wafanyikazi wa dayasisi hiyo, Padre Mbogo alisema kuwa michezo ina umuhimu katika kuunganisha taifa.

"Kaunti ya Nakuru ina makabila yote na tunaweza tumia michezo kama hii kuhubiri amani na uwiano miongoni mwa wakaazi," Mbogo alisema.

Wakati huo huo alitoa wito kwa wakristo kuzidi kuliombea taifa hili wakati ambapo Kenya inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.