Zaidi ya wanafunzi 50 kutoka eneo bunge la Mugirango magharibi wanaotoka kwenye familia maskini wamepata sababu ya kutabasamu baada ya wakfu wa Wakili Kemosi Mogaka kuwafadhili na hundi ya shillingi laki tatu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akihutubu kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Nyamira siku ya Ijumaa, Mogaka alisema alilazimika kuchukua hatua hiyo baada yake kugundua kuwa familia za wanafunzi husika hazikuwa na uwezo wakukidhi mahitaji yao. 

"Ni furaha ya kila mzazi kufahamu kuwa mtoto wake amefanya vyema kwenye mtihani na mimi kama mzazi nilipogundua kuwa wanafunzi hawa walikuwa wamepata alama 350 na zaidi niliguzwa sana nikaona sharti niwasaidie kwa mahitaji yao," alisema Mogaka. 

Wakili huyo aidha aliongeza kusema kuwa wakfu wa Kemosi Mogaka utaendelea kutoa ufadhili zaidi kwa wanafunzi wengine watakaofanya vyema mitahani ya kitaifa. 

"Elimu ni uhimu sana kwa ukuaji wa kiuchumi wa taifa lolote lile na sio kwamba hawa wanafunzi ambao tumewasaidia leo ndio tu watakao nufaika na mpango huu kwa maana tutaendelea kuwasaidia wanafunzi wengine zaidi ili nao wapate nafasi ya kuendelea kusoma," aliongezea Mogaka.