Share news tips with us here at Hivisasa

Miezi kadhaa baada ya makaburi ya Nakuru kaskazini kufungwa baada ya kujaa, shughuli sasa ziligeukia makaburi ya kusini mtaani Greenview.

La kushangaza ni kwamba makaburi ya kusini yameshawai jaa na kwa sasa ni kurudia tu kuzika miongoni mwa makaburi mengine ya awali.

Ni swala ambalo wakili Bernard Kipkoech Ng'etich anataja usumbufu wa wafu.

"Nashangaa sana ya kwamba watu wanazikwa mahala palipojaa awali kwa hivyo ni sawa na kusumbua wafu wengine," Ng'etich alisema.

Lakini usemi wa wakili hauchukuliwi kwa uzito kwani kila wiki miili inaendelea kuzikwa katika makaburi hayo.

Na kwa sasa shughuli za kupiga kaburi plasta zinaendeshwa katika makaburi haya kinyume na hapo awali.

James Kiri anayefanya kazi ya kupiga plasta katika makaburi hayo anasema kuwa kando na kusumbua wafu, yeye anaipenda kazi yake ya riziki ya kila siku.

"Mimi sitaki kusema eti ni kusumbua wafu bali najua ni riziki yangu," Kirii alisema.

Naye waziri wa afya kaunti ya Nakuru Dr Mungai Kabii alisema kuwa ni vyema kwa wananchi kukumbatia kuchoma miili.