Aliyekuwa mwenyekiti wa LSK kanda ya bonde la ufa wakili Bernard Kipkoech Ng'etich ameunga mkono sheria mpya inayopendekezwa na mkuu wa sheria kudhibiti makanisa na wahubiri walaghai.
Katika mahojiano, Ng'etich alisema kuwa wakati ni sasa kwani wakenya wengi wamelaghaiwa.
"Sio wahubiri wote wabaya, lakini kuna baadhi ambao sheria hii itawakabili vilivyo,"akasema wakili.
Itakumbukwa kuwa pendekezo hilo limeibua hisia mbalimbali miongoni mwa makundi ya kidini.
Wakati huo huo, Ng'etich alitoa wito kwa wabunge kubuni sheria ya kuzipa nguvu zaidi taasisi huru za kikatiba.
Kwa mujibu wake, taasisi zilizopo sasa hazina fedha za kutosha kujisimamia.
"Taasisi zilizopo za kikatiba zinafaa kupewa nguvu zaidi kujisimamia,"akaongeza wakili Ng'etich.
Matamshi yake yanajiri huku mrengo pinzani wa Cord ukishikilia kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi (IEBC).