Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakulima katika Kaunti ya Nyamira wamehimizwa kukumbatia teknolojia ya kisasa ili kuimarisha uzalishaji wa mazao yao.

Akiwahutubia wanahabari katika eneo la Manga siku ya Jumanne, mkulima tajika Daniel Metobo, anayekuza viazi, alisema kuwa mapato yake ya kuuza viazi yamekuwa yakiimarika zaidi kutokana nakukumbatia kwake kwa teknolojia ya sasa yakukuza mazao na mimea mbalimbali.

"Mapato yangu yamekuwa yakiimarika kila mwaka kutokana na kukumbatia teknolojia ya kisasa. Hatua hiyo imeniwezesha kuwasomesha wanangu na pia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo," alisema Motobo.

Motobo aidha aliwasihi wakulima kuasi tamaduni za zamani zakukuza mazao mbalimbali nakukumbatia teknolojia mpya hasa mbinu zilizo onyeshwa kwenye uwanja wa Nyamira wiki jana ili kuimarisha maisha yao.

"Ni himizo langu kwa wakulima kuasi mbinu zilizopitwa na wakati na kukumbatia teknolojia ya kisasa. Kuhusiana na dhana ya baadhi ya wakulima kuwa teknolojia ya ufugaji kuku na ng'ombe wa maziwa ni ghali, ningependa kuwafahamisha kuwa teknolojia hiyo sio ghali hata kidogo," alisema Metobo.