Share news tips with us here at Hivisasa

Wakulima wa viazi mjini Molo na Kuresoi wameteta kuwa wangali wananyanyaswa na madalali wa viazi kwenye eneo hilo kwani wamekosa kutii sharia ya upakiaji viazi.

Wakaazi hao walisema wafanyibiashara hawapakii viazi katika uzito wa kilo 50 kama jinsi ilivyopitishwa na serikali ya kaunti hiyo mwaka jana.

“Wafanyibiashara hawapakii viazi kwa mujibu wa sharia. Hizi viazi ziko na zaidi ya kilo 100 na wakulima hawana la kufanya kwani wanunuzi wako hivyo,” Peter Ngigi alisema.

Sheria hiyo ilipitishwa ili kuwalinda wakulima dhidi ya madalali ambao wamekuwa wakipakia viazi kupita vipimo.

“Sheria hiyo haitekelezwi kwani viongozi hapa wamekosa kushirikiana,” John Chirchir alisema.

Wakulima hao walisema serikali inafaa kuhakikisha kuwa swala hilo linarejelewa tena ili waweze kunufaika.