Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakulima wa majani chai kaunti ya Nyamira wamewaomba wakurugenzi waliochaguliwa katika viwanda mbali mbali katika kaunti hiyo kujitolea kufanya kazi ili kuwanufaisha kuendeleza kilimo cha mumea huo.

Wito huo umetolewa baada wakurugenzi kuchaguliwa wiki jana katika viwanda mbali mbali ili kuwahudumia wakulima ipasavyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari jumapili mjini Nyamira, wakulima hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kituo cha ununuzi cha majani chai cha Riyabe Kennedy Nyasato, waliwaomba wakurugenzi wote wapya kufanya kazi kwa minajili ya kuwanufaisha wakulima wa mumea huo katika eneo hilo.

Kulingana nao, wakurugenzi wnapaswa kutafuta soko nzuri ya zao hilo ili kupokezwa hela nyingi kwa kila kilo ikilinganishwa na fedha wanazopokea kwa sasa.

“Tunawaomba wakurugenzi wote tuliowachagua katika kaunti ya Nyamira wafanye kazi ambayo itatunufaisha sisi wakulima,” alisema Nyasato.

“Tunawaomba watafute soko ya majani chai yetu ili tuanze kupewa pesa nyingi kwa kila kilo ili tufaidike na kilimo chetu,” aliongeza.

Wakati huo huo, wakulima hao waliwaomba wakuh hao kuhakikisha kwamba barabara zote zinazoelekea kwa vituo vya ununuzi vya majani chai zinakarabatiwa, majani chai imepimwa uzani na kuchukuliwa viwandani kwa wakati unaofaa ili kutowasababishia hasara, aliongezea Beatrice Mokeira.