Share news tips with us here at Hivisasa

Ili kukabiliana na visa vya utumizi wa dawa za kulevya katika kaunti ya Mombasa ni lazima kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuwashauri vijana athari ya utumizi wa mihadarati na vileo.

Mkurugenzi wa Bodi ya kupambana na mihadarati na vileo nchini Nacada Sheikh Juma Ngao amesema kuwa vijana wengi wameathirika na utumizi wa mihadarati unaochangiwa na baadhi ya walanguzi mkuu na lazima wakabiliwe kisheria.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Sheikh Ngao amesema kuwa iwapo wadau hao wataungana na kuhakikisha kuwa vijana wameshauri vyema basi itakuwa rahisi kwa vijana hao kuwataja walanguzi wakuu na kukabiliwe ili kusitisha vijana kuathirika na mihadarati.

“Tunawaomba wadau mbalimbali kuungana na kuwashauri vijana jinsi ya kujingeza na mihadarati na maafisa wa polisi kujitkeza waziwazi kuwatia nguvuni walanguzi wakuu wa mihadarati kwani kwa kufanya hivyo basi kutawaakoa vijana wetu,” alieza Sheikh Ngao.

Amesema kuwa takwimu inaonyesha kuwa kaunti ya Mombasa ndio inaongoza kwa vijana wengi waliyoathirika na utumizi wa dawa za kulevya na lazima jinamizi hilo kushughulikiwa mara moja ili kuwanasua vijana wadogo katika janga hilo la utumizi wa dawa za kulevya.

Mkurugenzi huyo wa bodi ya Nacada ambaye pia ni kiongozi wa dini ya Kiislam ameahidi kukabiliana na janga hilo ili kuwanasua vijana wengi kaunti ya Mombasa na eneo zima la Pwani.