Share news tips with us here at Hivisasa

Walemavu katika eneo bunge la Changamwe wamefaidika pakubwa na ufadhili wa viti vitakavyo wasaidia katika kutekeleza shughli zao za kila siku.

Viti hivyo vilitolewa siku ya Jumamosi na baraza la kitaifa linaloshughulikia walemavu humu nchini.

Akizungumza na wanahabari wakati wa kukabidhi viti hivyo, Sara Ayiecho, afisa katika baraza la kitaifa la walemavu nchini alisema jukumu la shirika hilo ni kuhudumia walemavu bila ubaguzi.

Ayiecho aliongeza kuwa lengo hasa ni kupunguza umaskini kati ya walemavu.

Aidha, alisisitiza kuwa watafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa walemavu wote katika sehemu hiyo wanapata misaada kwa wakati ufao.