Share news tips with us here at Hivisasa

Zaidi ya walimu 40 wakuu wa shule za upili za umma Kaunti ya Mombasa wametia saini kandarasi ya utendakazi, licha ya baadhi hao kuibua tetesi kuwa mpango huo huenda ukawakandamiza.

Mkurugenzi mkuu wa Tume ya kuajiri walimu TSC Kaunti ya Mombasa Ibrahim Rugut amesema kuwa kandarasi hiyo itasaidia kuimarisha sekta ya elimu katika shule za umma.

Rugut amewataka walimu hao kutokuwa ha hofu kwani kandarasi hiyo ni ya utendakazi, bali sio ya kuajiri huku akisema kuwa wale wanaosusia mpango huo huenda wakakosa nafasi za kupandishwa vyeo.

“Ninawahimiza walimu wakuu ambao wako na tashishwi kuondoa hofu kwani kandarasi hiyo aihusiani na uajiri bali kujua juhudi katika utendakazi na kuimarisha sekta ya elimu,” alisema Rugut baada ya kukutana na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumamosi.

Zoezi hilo lililoongozwa na mkurugenzi huyo linapania kuimarisha viwango vya elimu Kaunti ya Mombasa na kuorodhesha matokeo bora ya mitihani ya kitaifa.