Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery amesema kuwa waote waliotiwa mbaroni Maela Naivasha wakati wa mzozo wa shamba la Ng’ati wataachiliwa bila kutozwa dhamana.

Akionge mjini Naivasha Jumatano, Nkaissery alisema wote waliotiwa mbaroni wanafaa kuachiliwa mara moja kwani walikuwa wakitetea haki kwenye maandamano ya wanachama wa Ng’ati.

“Wale wote walikamatwa wataachiliwa bila kutozwa chochote. Hakuna hiyo mambo ya bondi ya milioni moja,” alisema Nkaissery.

Watu kadhaa walitiwa mbaroni wakati wanachama wa Ng’ati walifanya maandamano kulalamikia uuzaji wa ekari elfu tatu na baadhi ya wakurugenzi bila ya kuwahusisha wanachama.

Baadhi ya wale waliokamatwa ni MCA wa eneo hilo Kariuki Mujina baadhi ya washukiwa wengine. Waziri Nkaissery alizuru eneo hilo akiandamana na mbunge John Kihagi wa Naivasha.