Zaidi ya vijana ishirini wanachama wa kundi la M.R.C wamejisalimisha kwa maafisa wa usalama na kuomba radhi kuwa wamekubali kubadilika na hivyo kutaka msaada.
Kulingana na Omar Abdala, ambaye ni mmoja wa waliojisalimisha, vijana hao hujiunga na kundi hilo baada ya kuahidiwa kuwa watapata ufadhili wa kujiendeleza maishani.
“Kuna baadhi ya viongozi haswa wanasiasa ambao hutumia sisi vijana kutekeleza mahitaji yao kwa ahadi kuwa tutafaidika na kutoweka baada ya kupata wanachotaka,” alisema bwana Abdala.
Hata hivyo, mshirikishi wa eneo la Pwani Nelson Marwa amewaomba wananchi kuwakubali katika jamii kwa kuwa wameonyesha kuwa wako tayari kubadilika na kuwataka kushawishi wenzao ambao bado wanashiriki na kundi hilo ili kujitoa.
Picha: Vijana wa kundi la MRC wakiwa mahakamani katika kesi ya hapo awali. Vijana kadha wa kundi hilo walijisalmisha na kutaka kupokea msaada. thestandard.co.ke