Wanafunzi takriban 132 kutoka shule ya upili ya Limuko eneo bunge la Bahati wamefaidika na basari.
Wanafunzi hao walipata basari ya 124, 000 siku ya Alhamisi kutoka kwa afisi ya mbunge wa eneo hilo Kimani Ngunjiri.
Ufadhili huo ulipatiwa wanafunzi hao ambao ni kutoka familia maskini kwenye wadi ya Kabazi.
Mbunge Kimani Ngunjiri alisema kuwa afisi yake imejikakamua kuhakikisha wanafunzi kutoka familia maskini wamefaidika ili kuendeleza ndoto yao ya elimu.
Waliofaidika walisifia hatua ya mbunge huyo.
“Nimefurahi angalau karo yangu imepungua na sasa wazazi wangu watapambana na hiyo nyingine,” Peter Kamau alisema.