Zaidi ya wanafunzi 260 wa shule ya msingi ya Migujini huko Bamba kaunti ndogo ya Ganze,kaunti ya Kilifi wanalazimika kusoma chini ya miti baada ya paa la madarasa kusombwa na upepo.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Omar Mudzomba tukio hilo halikuathiri mwanafunzi yeyote kwani wanafunzi walikuwa tayari wameenda nyumbani baada ya masomo.
Aidha, Mudzomba amesema kuwa kwa sasa shule hiyo inahitaji mfadhili ama serikali kuisaidia katika kukarabati paa la majengo ya shule hiyo kwani mvua ya masika huenda ikaanza hivi karibuni kama ilivyotangazwa mapema wiki hii na idara ya hali ya anga nchini.
Mudzomba hata hivyo amemtaka mwakilsihi wa wadi ya eneo hilo pamoja na Mbunge wa Ganze Peter Shehe kuingilia kati na kuwasaidia na raslimali za kukarabatia madarasa yalioathirika na upepo huo.
Mudzomba pia ameongoza kuwa ni jumla ya shillingi laki mia mbili hamsini zinazohitajika kwa sasa ili kukarabati majengo hayo.